Serikari ime shauriwa kupiga marufuku usambazaji wa DVD zenye maneno ya Uchochezi ili kuepuka kuenea kwa chuki na mivutano ya kiimani isiyo na tija.
Wananchi hao ambao
wameelekeza kilio chao moja kwa moja kwa
Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania
(TCRA) na Jeshi la Polisi, wanasema
mamlaka hizo zinapaswa kuwajibika kwa
kuwashughulikia watu wanaosambaza picha
za video na mahubiri yaliyopo katika mfumo
wa sauti (Audio), kwa maelezo kwamba
nyingi ya video hizo zimejaa maneno ya
kichochezi yanayoweza kuamsha hasira na
hisia za kidini.
Mmoja wa wananchi hao aliyejitambulisha
kwa jina la Mbati Tuta kutoka wilayani
Newala, anasema upigaji marufuku wa
biashara hiyo utasaidia kwa namna moja au
nyingine, kupunguza uchochezi
unaosambazwa kupitia mahubiri yenye
maudhi kwa imani za dini nyingine.
“Tukubali au tukatae, usambazaji na uuzwaji
huu wa DVD na kanda zenye mahubiri ya
aina hii, unaweza kuwa moja kichocheo cha
uvunjifu wa amani na hasa katika kipindi hiki
cha kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu…ni
vyema Serikali ikajitahidi kukomesha
viashiria hivi vya uvunjifu wa amani
vinavyoanza kujitokeza sasa,” anasema
Tuta.
Kwa mujibu wa mwananchi huyo, mara
nyingi matukio ya vurugu za kiimani
yanayotokea ndani na nje ya Mkoa wa
Mtwara, yamekuwa yakihusishwa na hisia
chafu za kisiasa.
....kwa nyakati na
maeneo tofauti mkoani humo, baadhi ya
wananchi wamekwenda mbali kwa kuiomba
Serikali ipige marufuku utayarishaji wa
mikanda ya aina hiyo katika studio bubu
pamoja na uuzwaji wake unaofanyika kupitia
maduka ya muziki pamoja na
wafanyabiashara wadogo maarifu kwa jina la
machinga wanaoziuza mitaani, huku
wakitaka wahubiri wa mahubiri hayo
yanayochochea chuki za kiimani, kuendesha
mahubiri yao hayo ndani ya Misikitini na
Makanisa.
“Uwepo wa gesi asilia hapa Mtwara,
umewafanya baadhi ya watu wahubiri
mambo ya uchochezi badala ya amani.
Serikali isipoyadhibiti mambo haya mapema,
yanaweza kuibua vurugu na hisia za kibaguzi
za nani anastahili kuwekeza katika sekta
hiyo ya gesi na nani hatakiwi kuwekeza,
matokeo yake itakuwa ni vurugu,”
anasema
mwananchi mwingine, Mkomwa Amalia,
mkazi wa Kijiji Mdenge, Kata ya Likombe
katika Manispaa ya Mtwara/Mikindani.
.... “Pamoja na ukimya wa Serikali na udhibiti
wake kwa vyombo vya habari kutoeleza hali
halisi ya machafuko yanayoendelea kutokea
nchini, bado harufu mbaya huku kusini
inatisha, tunaomba kabla ya kuingia kwenye
mchakato wa Uchaguzi Mkuu, Serikali
ihakikishe inadhibiti hali hii,” anasema
Amalia na kuongeza:
“Nani asiyejua kwamba kujadili dini ya mtu
mwingine kwa kukashifu, ni mambo
yasiyotakiwa ndani ya jamii zetu ili kuepusha
shari na kudumisha amani? Sasa kwanini
hali hii inaachwa bila kudhibitiwa?”
Imeelezwa kwamba baadhi ya kumbi za
mikutano na starehe mkoani humo zimekuwa
zikitumika kuonyesha mikanda ya video
yenye mihadhara inayochochea hisia za
kidini, bila kujali madhara jamii yanayoweza
kutokana na mahubiri hayo.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limeeleza
kutokuwa na taarifa ya kuwepo kwa kanda
hizo za mahubiri ya kichochezi, huku likiahidi
kufuatilia suala hilo.
Kumbukumbu zinaonyesha kwamba mwaka
2013 ziliibuka hisia za imani za kidini,
zilizoambatana na umwagaji wa damu
zikitokana na sababu uchinjaji kitoweo.
Serikali ilikemea tabia ya kuingilia imani za
dini nyingine pamoja na kuwataka wananchi
kudumisha amani iliyopo.
Aidha, Serikali iliwataka wakuu wa mikoa
nchini kuondoa woga na kusimama kidete ili
kukomesha vurugu zilizokuwa zimeanza
kushika kasi nchini, zikienezwa na tofauti za
nani ana haki ya kuchinja kati ya wenye
imani ya dini ya Kiislamu na Wakristo.
MJUMBE BLOG Tunashukuru kwa kututembea.
Karibu tena!
Upate huduma zetu mbalimbali.
Jsssj
Jssjs
Jjjj
Post a Comment