Mwandishi maarufu kutoka Algeria, Asia Jabbar
amefariki akiwa na miaka 78 mjini Paris.
Kulingana na habari ya radio ya Algeria,Asia
Jabbar aliaga dunia akiwa hospitalini mjini Paris
usiku wa Ijumaa.
Jina asili la mwandishi huyu mwenye asili za
Uarabu lilikuwa Fatma Zohra Imalayen. Alikuwa
mgombea wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi mwaka
2009 na kuchaguliwa mwandishi bora zaidi katika
Chuo cha Fasihi cha Ufaransa (Académie
Française).
Alibandikwa lakabu ya "mwanasheria wa
wanawake" kutokana na juhudi zake katika
maendeleo na haki za wanawake ulimwenguni.
Mwaka wa 1957, kitabu chake cha kwanza cha
riwaya cha "La Soif" (Kiu) kilimtambulisha katika
dunia ya uandishi na pia kumpa ushindi wake wa
kwanza kutoka jarida la Fasihi la L'algerienne
nchini Algeria.
Jabber ambaye aliongoza Tawi la Fasihi ya
Kifaransa katika chuo kikuu cha Algeria, alifunza
somo la historia katika chuo hiko kikuu.
Vitabu vya marehemu Asia Jabber kama vile
"Baba sina nafasi nyumbani" vimefasiriwa katika
lugha mbalimbali kote ulimwenguni.
MJUMBE BLOG
Tunakupongeza kwa kutumia huduma zetu.
HONGERA;
Karibu tena.
Post a Comment