Unknown Unknown Author
Title: UJENZI WA VYOO BORA VIJIJINI BADO NI CHANGAMOTO....!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pichani ni choo ambacho kinatumika kama kawaida. Ujenzi wa Vyoo vijijini bado unachangamoto kubwa sana. Wananchi wengi hawana Ufahamu w...

Pichani ni choo ambacho kinatumika kama kawaida.


Ujenzi wa Vyoo vijijini bado unachangamoto kubwa sana.
Wananchi wengi hawana Ufahamu wa kutosha ili waweze kuelewa Umuhimu wa kujenga Vyoo vya kisasa na vya kudumu...

Wanakitazama Choo ndani ya Makazi yao kama sio jambo la lazima wala Lenye Umsingi wowote...
Kwani nyumba bila choo kwao ni jambo la kawaida.

Ufahamu mdogo wa Umuhimu wa vyoo ndani ya jamii umesababisha kufanyike jitihada za dhati na serikari ambapo wadau mbali mbali wame kuwa wakihamasisha ujenzi wa choo bora ambacho kitazingatia kanuni zote za afya.

Kutekeleza hilo tayari kuna utaratibu wa Kunawa mikono kila unapo toka chooni ambao ume wekewa juma maalum kwa mwaka.

Pia kuna wadau mbali mbali ambao hufadhili ujenzi wa vyoo imara ndani ya jamii hasa vijijini.
Miongoni mwa mashirika yasiyo ya kiserikari yanayo jishughulisha na UHAMASISHAJI WA UJENZI WA VYOO nyanda za juu kusini mwa Tanzania ni SHIPO...

Hawa wana makao yao makuu katika mkoa wa njombe pamoja na kutoa huduma mbali mbali za jamii ikiwemo kusaidia ujenzi wa mabweni kwa ajili ya watoto wa kike,Usambazaji wa maji vijijini,wame kuwa waki himiza na kuhamasisha Ujenzi wa vyoo bora pia.


MJUMBE BLOG tuna amini kuwa NYUMBA BORA NI PAMOJA NA CHOO BORA PIA! Kwa maana fupi Nyumba ni choo.
Rai yetu;Tujenge nyumba bora Lakini Tusisahau ujenzi w vyoo bora kwa manufaa ya afya zetu.


Ndugu mdau wa MJUMBE BLOG Mtandaoni:
Tunashukuru kwa kutumia huduma zetu.
Karibu tena.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top