UN yailaumu Tanzania kwa hali ilivyo DRC
Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za
Tanzania na Burundi kuhusiana na hali
katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Ripoti mpya ya kundi la wataalamu wa
umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu
Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa
kundi la waasi wa FDLR kuandaa
mikutano nchini humo.
Imeeleza pia kwamba wanajeshi wa
Burundi wametekeleza unyanyasaji wa
kingono.
Taarifa hiyo ya Umoja wa mataifa
inasema kuwa tangu mwaka wa 2013,
viongozi wa FDLR na baadhi ya washirika
wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa
wakikutana nchini Tanzania. Credit:BBC
MJUMBE BLOG
Tunakushukuru kwa kuweza kututembea.Endelea kutufuata mtandaoni kwa habari Matukio zaidi.
Post a Comment