Unknown Unknown Author
Title: ZIARA YA JOACHIM GAUCK IMELENGA ZAIDI MAHUSIANO YA KIBIASHARA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa Ujerumani Joachim Gauck yuko nchini Tanzania kwa ziara rasmi ya siku sita. Kiongozi huyo amepokewa na mwenyeji wake Rais Jakay...

Rais wa Ujerumani Joachim
Gauck yuko nchini Tanzania
kwa ziara rasmi ya siku
sita. Kiongozi huyo
amepokewa na mwenyeji
wake Rais Jakaya Kikwete
wa Tanzania.

Rais Gauck ambae
anatarajiwa kufanya
mazungumzo na matabaka
mbalimbali ya viongozi
nchini Tanzania amewasili
jana jioni. Baada ya hafla
ya mapokezi iliyofanyika
katika Ikulu ya Dar es
Salaam viongozi hao wawili,
Rais Kikwete na Gauck,
walifanya mazungumzo ya
faragha, na baadae
kukutana na waandshi
habari.

Pembezoni mwa
mazungumzo ya viongozi
hao wawili, kulifanyika pia
mazungumzo ya wake wa
marais, Mama Salma
Kikwete na Bibi, Daniela
Schadt, mke wa rais Gauck.
Mke huyo wa Rais Gauck
atazitembelea taasisi tatu,
ikiwemo WAMA,
inayosimamiwa na rais mke
wa Rais Kikwete na kisha
hospitali ya tiba maalum za
viungo ya CCBRT ya jijini
Dar es Salaam.

Pamoja na tiba ya macho
hospitali hiyo inafanya
upasuaji kwa watoto wenye
kuzaliwa na kasoro ya
kinywa, maarufu kama
midomo sungura na tatizo
la fistula kwa wanawake.
Katika ziara hiyo ya siku
sita pamoja na mambo
mengine Rais Gauck
anapata fursa ya
kuzungumza na wadau
kutoka katika asasi za
kiraia.
Matarajio ya Watanzania
Mkurungezi wa Idaya ya
Habari na maelezo ya
nchini Tanzania anasema
kikubwa kinachotarajiwa
kwa Watanzania wengi ni
kuimarika kwa ushirikiano
baina ya mataifa hayo
mawili hasa kwa kuzingatia
fursa ziliopo za
maendeleao.

Historia ya uhusuano wa
Ujerumani na Tanzania
Kihistoria Ujerumani na
Tanzania zimekuwa na
uhusiano wa karibu tangu
zama za Ukoloni.
Tanganyika ilikuwa koloni
la Ujerumani kwa takribani
miaka mia moja iliyopita.
Ushirikiano huo umekuwa
katika nyanja tofauti
kuanzia kisiasa,
kiutamadauni, kiuchumi na
hata katika suala la imani
za kidini. Lakini
mchambuzi kutoka wakfu
wa Kijerumani wa Konrad
Adenauer i, ofisi ya Dar es
Salaam, Richard Shaba
anasema kwa hivi sasa
mambo yamebadilika
kabisa " Ujerumani
haijihusishi tena na
Ukoloni.
Baada ya Tanganyika kuwa
taifa huru, mahusiano ya
kidiplomasia yalianza baina
yake na Ujerumani.

Kulikuwa na wakati mgumu
mwaka 1964 pale ambapo
Tanganyika na Zanzibar
zilipoungana. Zanzibar
ilikuwa na uhusiano na
Ujerumani Mashariki na
Tanganyika ikiegemea
Ujerumani Magharibi.
Wakati ule wa Vita Baridi,
Ujerumani Magharibi
ilikataa washirika wake
wawe na uhusiano na
Ujerumani Mashariki. Rais
wa Tanzania Hayati Julius
Kambarage Nyerere aliona
hayo kuwa ni kuingilia
masuala ya ndani ya taifa
lake. Na maneno yake
katika kuepusha hilo
yalikuwa "Huwezi
kutuchagulia marafiki".
Katika kusimamia kauli
yake hiyo aliagizia
Wajerumani wote
waondoke nchini mwake,
isipokuwa wafanyakazi wa
Ubalozi.

Wakati mwingine
mgumu
Awamu nyingine ngumu
katika uhusiano wa
Ujerumani na Tanzania
ilikuwa mwaka 2013.
Kipindi hicho Tanzania
ilikataa kumpokea
aliyeteuliwa kuwa balozi
wa Ujerumani nchini humo,
pasipo kutaja sababu
yoyote, ingawaje sheria za
kimataifa zinaruhusu nchi
yenye kupokea balozi kuwa
na haki ya kufanya hivyo.
Wizara ya mambo ya nje ya
Ujerumani iliulezea uamuzi
huo kuwa usioeleweka.
Watanzania wanaitambua
Ujerumani katika ujenzi wa
demokrasia ya taifa lao.
Umuhimu wa ziara ya
Gauck
Ziara ya siku tano ya rais
Gauck inakoja baada ya
kushindikana kwa ile ya
mtangulizi wake Christian
Wulff ambae alishindwa
kukamilisha ziara yake
nchini Tanzania baada ya
kujiuzulu siku chache kabla
ya kukamilisha ziara kama
hiyo.

Ziara hiyo ina
umuhimu wa kukuza
ushirikiano wa
kibiashara,kiuchumi na
kisiasa baina ya mataifa
yote mawili. Hata hivyo
mchambuzi na mtaalamu
wa masuala ya siasa kutoka
Tanzania Profesa Mwesiga
Baregu,amesema uhusiano
wa kibiashara kati ya
matiafa hayo mawili bado
mdogo, lakini unakuwa.

Anasema wawekezaji wa
Kijerumani wanaonesha
kuvutiwa na nia ya
uwekezaji katika rasilimali
mpya ya gesi nchini humo.
Naye Richard Shaba wa
Konrad Adenauer anasema
umuhimu wa nishati
mbadala nchini Tanzania
unaweza kuunganisha
mataifa hayo mawili katika
mipango ya siku za usoni.
Ameongeza kwamba
Ujerumani ina ujuzi
mkubwa katika sekta hiyo
yenye kujumuisha nishati
itokanayo na jua, upepo na
maji, nishati ambazo
vyanzo vyake vinapatikana
kwa wingi nchini Tanzania
Mwandishi: Sudi Mnette/
DW
Mhariri:Mohammed Abdul-
rahman.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top