Unknown Unknown Author
Title: NI VIGUMU VITA KUSITISHWA SUDANI KUSINI
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  Msemaji wa jeshi amesema kuna matumaini madogo ya kusitishwa kwa mapigano Sudani kusini kwa sasa.Kiongozi wa waasi Riek Machar amese...

Msemaji wa jeshi amesema kuna matumaini madogo ya kusitishwa kwa mapigano Sudani kusini kwa sasa.Kiongozi wa waasi Riek Machar amesema wapiganaji wake bado wanashikilia eneo kubwa la kaskazini mwa nchi huku majeshi ya serikali yakisema yameukomboa  mji wa Malakal na wamezingira eneo la Bentiu,mji mdogo wa jimbo la Unity.

Rais Salva Kiir amesema yupo tayari kusitisha mapigano mara moja lakini hasimu wake bwana Machar amesema mazugumzo zaidi yanahitajika kukubaliana  kusitisha mapigano na kwamba yupo tayari kufanya mazungumzo iwapo serikali itakua tayari kuwaachia huru wanasiasa 11 wanaomuunga mkono ambao walikamatwa wakati vurugu zilipotokea.
chanzo:bbc

Na mjumbe jr
Morogoro

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top