Unknown Unknown Author
Title: ISOME HOTUBA ALIYO ITOA ZITTO KABWE KWA MARA YA KWANZA TANGU AVULIWE MADARAKA YOTE NA KAMATI KUU YA CHADEMA!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Leo nina Furaha kubwa sana  kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbai kuwasalimu wana nchi wenzangu! Nahii si sala...

Leo nina Furaha kubwa sana  kwani baada ya safari ndefu na yenye changamoto nimerudi nyumbai kuwasalimu wana nchi wenzangu! Nahii si salaam za kawaida bali nawasalimu kwa Salaamu za kidemokrasia,uadilifu,Uzalendo na uwajibikaji.Nawasalimu si kama mbunge bali kama mwana wenu wa Kigoma! Napopote niendapo Najivunia kujitambulisha kama Mtanzania;Kama Mwenyeji wa mkoa wa Kigoma na zao la ujiji.Tuna mengi ya kujivunia kama Taifa lakini ujiji na watu wake mna nafasi ya pekee katika Historia.Watu wa ujiji mlipokea harakati za kupokea uhuru wa nchi yetu mapema kabisa mapambano ya Uhuru yalipo anza.Watu wa ujiji mlikuwa wa kwanza kabisa kuupokea mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.Na jimbo la Kigoma mjini lilikuwa miongoni mwa majimbo ya mwanzo kutoa mbunge wa CHADEMA mwaka 1995,kabla ya hapo mlitoa madiwani wengi mwaka 1994.

Wakati Watanzania wengi wakiwa wanajiuliza mara mbili mbili kuhusu kujiunga na vyama vipya vilivyo anzishwa watu wa Kigoma Ujiji hamkusita kupokea Mabadiliko,Wengi wame poteza Maisha yao,Wengine kazi zao, na wengine hata Ndoa zao katika kupata Mbegu ya mabadiliko katika nchi yetu.Nawataka msichoke,Wekeni nguvu mpya katika kusimika mabadiliko kwani bado kazi ya kuimarisha Demokrasia katika nchi yetu haija isha na inahitaji Uvumilivu,Kusameheana, na Kuaminiana.
 Na nchi yetu Tanzania ni nchi inayo onesha  uwezo mkubwa katika Kupendana,Kuaminiana,Kuvumiliana na hata Kusameheana.Nahaya si maneno tu ninayo yazungumuza kama mwana Siasa.Hii ni hali halisi na maisha niliyo yaishi mfano nilipokuwa nina kuwa na kusoma katika Shule ya Msingi Kigoma na baadaye Shule ya Sekondari Kigoma malezi yangu yamekuwa yaki ongozwa na jamii nzima ya Kigoma.Nime kuwa nikiwaeleza rafiki zangu nilio kutana nao kwenye masomo na kwenye Siasa kwamba nime anza kuvaa viatu kwa mara ya kwanza nikiwa darasa la Tatu.Viatu vilivyo itwa 'asante Salim vilivyo kuwa vinatengenezwa na kampuni ya Bora shoe vilinunuliwa na mama Coretha Furugunya ambaye tulikuwa tuna kaanaye mta mmoja wa Kisangani mwanga.Mama Coretha Hakuninunulia viatu kwasababu alikuwa na uwezo mkubwa,la hasha alifurahishwa na matokeo yangu ya mtihani wa darasa la pili kwenda darasa la tatu.Nina amini kitendo cha mama huyu ni ushahidi wa uungwana,Upendo na hata Uwajibikaji ambao tunao sisi watanzania.Uwajibikaji kwani alichukua jukumu la kunilea ingawa hakuwa mzazi wangu lakini aliona kuwa kama mwana jamii ananafasi kubwa katika kuwaendelez watoto wote.Jamii hii ya Kigoma ilinifunza kuwa nikijitahidi na kukazana kwa bidii kwenye masomo na majukumu nitafanikiwa.Siwezi kulisahau Somo hili katika maisha yangu na ni somo hili nijitahidi kwa kadri ya uwezo wangu kuwatumikia kwa uadilifu na mafanikio ya hali ya juu sana.Nikiwa nime jaa matumaini haya kuhusu wana nchi wenzangu,leo nataka niwakumbushe kwanini kama jamii Tuli chaguo kufuata njia ya Kidemokrasia.Demokrasia inamaana pale inapo tumika kuleta mabadiliko chanya kwenye maisha ya wana nchi maisha yanayotakiwa ni yale yanayo mwezesha mwana nchi kujipatia stahili zake kama vile huduma za Afya,ElimuMji na Miundo mbinu.Demokrasia haina maana pale wana nchi wanapo kufa njaa kwa kukosa ajira na kukuza Umasikini.Demokrasia inahusu maendeleo.Tumejitahidi kwa upande wetu kuutoa mkoa wa Kigoma kutoka mikoa isiyo na miundo mbinu kabisa ya maendeleo mpaka kuwa mkoa unao tumika kama mfano kwenye miradi mingi ya Maendeleo,Ikiwemo daraja la malagarasi,Uwanja wa ndege wa Gombe-Mahale,Barabara za lami na upanuzi wa Bandari ndogo na ujenzi wa kituo cha usafirishaji mwandiga.Asije mtu kusema yeye ndiye kafanya haya.Haya ni matunda ya nyie watu wa Kigoma kupokea Demokrasia na bila woga kuchagua viongozi wenu bila kujali vyama bali kwa kuangalia Uwezo.Haya ni matokeo ya viongozi wenu kupaza sauti yenukwenye baraza la Taifa,bunge.Haya ni matunda ya uvumilivu wenu na uamuzi wa kutaka maendeleo.Juhudi hizi ni lazima ziendelezwe kwa bidii zote ili kuhakikisha kuwa nafasi ya mkoa wa Kigoma katika Uchumi wa Tanzaniainaonekana dhahiri na hivyo kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwa kitovu cha biashara katika nchi za maziwa makuu.
Lakini pia tukumbuke kuwa Demokrasi ni Uwajibikaji.Katika kipindi cha utumishi wangu kwenukutokana na maleziniliyo yapata kutoka kwenu,nime kuwa mstari wambele kuhakikisha kuwa Serikari inawajibikakwa wana nchi.Nakumbuka wakati napambana kuhusu sheria mbovu ya madini kuna watu hapa nyumbani walisema 'sasa huyu kawa mbunge wa Taifa lakini watu wengi zaaidi wakasema Tume mtuma Dodoma kusemea watanzania wote na sio Kigoma tu.Tuliweza ndani ya miaka mitano kufanya mabadilko makubwa sana kwenye sera ya madini  na sheria ya madini ambapo baadhi ya mambo ambayo yalikuwa hayafikiriki sasa yame tungiwa sheria ikiwemo serikari kuwa na his kwenye migodi Tanzanite kumilikiwa na Watanzanu sio Chini ya asilimia 50 na kuzuia kabisa wageni kuchimba vito vya Thamani.Uwajibikaji ulipelekea kumshinikiza Rais  kufanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri. kwa kuwafukuza mawziri wanne mwaka jana. Hii ilitokana sio tub kuwa na hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu bali ushiriki wa wana nchi kwa kupiga simu kupitia simu na mitandao ya kijamii ambapo wabunge walishinikizwa kuweka saini kwenye karatasi za kumtoa waziri mkuu.Toka wakati huo kumekuwa na utaratibu sasa ambapo wabunge hawaoni taabu kutaka uwajibikaji wazi wazi ilin kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma.Ni hivi jana tumeshuhudia mawaziri wanne wame jiuzuru kutokana na kashifa ya tokomeza ujangili iliyo ibuliwa na ripoti  ya kamati ya bunge.Mabadilko haya ni hatua muhimu katika kuiamarisha Demokrasia yetu.
Kutoa Aminiana Ni dhahiri kuwa kuto aminiana katika nchi yetu kume kuwa kwa kiasi kikubwa.
Taarifa za kitafiti zina onesha kuwa katika kila watu kumi,watu nane hawa aminiani.Nichangamoto kubwa sana.Wana nchi wame acha kuwa amini wana siasa na wana siasa wame acha kuaminiana wenyewe kwa wenyewe.Hivi sasa uongo una geuzwa kuwa ukweli na Ukweli umekuwa ni uongo.hivi sasa ukitaka kuwa mwanasiasa maarufu lazima ujue jinsi ya kudanganya na ukitaka uitwe mwana siasa msaliti inabidi useme ukweli.Kukosekana kwa uaminifu na kuaminiana imekuwa in kama kansa katika siasa zetu.Itachukua muda mrefu sana kujenga demokrasia imara katika nchi yetu kama hatuta pata jibu la changamoto hii ya kuto aminiana na kugeuza uongo kuwa ukweli na ukweli kuwa uongo.Hivi sasa ukweli umekuwa unatengenezwa badala ya kutafutwa.Ni Mjajanga.Juzi mwanasheria mkuu alielekeza shutuma kwangu kwamba siku shirikiana na kamati maalum iliyoundwa na bunge kufuatilia mabilioni ya Uswisi na kwamba chini ya kiapo nilisema kwamba sina majina ya watu wenye akaunti huko Uswisi.Huu ulikuwa ni uongo.Niuongo kwasababu niliwapa wajumbe wa kamati maalum maelezo na taarifa nyingi sana kuhusu utoroshwaji wa fedha nje ya nchi na umilki wa mali nje ya nchi kinyume cha Sheria.Niuongo kwasababu mimi kutotaja majina  haya haina maana sina majina,bali ni kwamba nina heshimu utaratibu na nime achia vyombo husika vikamilishe uchunguzi.Kwani mimi kama mtu binafsi nikianza kuchukua majukumu ya taasisi nia weza kutia dosari harakati hizi muhimu na hata kupelekea mchakato mzima kuvurugika sita ingia mtego huu.Lakini hatua hii ya mwanasheria mkuu imenipelekea kujiuliza maswali menge kwa mfano uongo kama huu ulifanywa kwa malengo gani? Na ninajikuta hata mimi nina ingiakatika hali nisiyo iamini ya kuto AMINIANA.
Lakini mtambue kuwa kuto aminiana kuna leta kutovumiliana.Hivi sasa kuwa na mawazo tofauti katika vyama vya siasa au hata asasi za kijamii ni uhaini.Lakini bila kuenzi tofauti za mawazo na uhuru wa mawazo hatwezi jenga vyama imara wala Tanzania Imara.Demokrasia imara ni zao la Tofauti za kimawazo na uhuru wa mawao.Kama hatuwezi kujenga vyama vinavyo rutubisha uhuru wa mawazo na tofauti za mawazo Tutajenga Taifa lenye watu wenye kuogopa na walio jaa woga.
Wanachama wanapo ogopa uongozi ni udikteta;Lakini Uongozi unapo ogopa Wana chama ni Demokrasia.Bila Demokrasia ya uwazi na kuvumiliana tutakuwa Taifa la kidikteta;Lazima vyama vya siasa viongozwe kwa namna ile ile ambayo taifa litaongozwa.
Demokrasia bila kuaminiana,Demokrasia bila kuvumiliana, siyo Demokrasia ya kweli.Juzi nilipo ingia bungeni kwa mara ya kwanza baada ya matukio kadhaa yanyo endelea kwenye chama chetu nili kaa pamoja na mbunge Tundu Lissu.Wabunge wengine walidhani tutarushiana ngumi na badala yake ikawa ni vicheko na mazungumzo.Hii ni kwasababu sina Chuki na mtu yeyote yule.Mme nifunza kuto jenga chuki na mtu yeyote na badala yake kuchukua kila tukio kama changamoto ya maisha.Siasa ni kupambanisha mawazo tofauti hatimaye kutafuta Suruhu ya Pmoja.Na siasa ina misingi yake ambayo sisi wanasiasa huwa tuna isahau kwa makusudi.Msingi wa siasa ni kuwa inapaswa kuleta unafuu wa maisha kwa wan nchi na sio marumbano tu ya kurushiana maneno na kuzushiana ili kujijengea umaarufu wa kisiasa.Siasa si kuwekeana chuki na kuonesheana Ubabe.N hapo inabidi muelewe wana kigoma ,munapo ambiwa kuwa ninapo fuatilia mabilion ya Uswisi nina tafuta Umaarufu,ni Uongo! Munapo Sikia eti kukataa kwangu kuchukua posho ni Unafiki na kujitafutia umaarufu ni Uongo,kinacho nisukua kufanya vyote hivi ni ninyi.Nina sukumwa kila ninapo ona watoto wana tembea bila viatu,Kila niapo ona akina mama wana poteza maisha yao katika uzazi,kila ninapo ona vijana ambao hawana uhakika wa kupata hata mlo mmoja kwa siku kwa kukosa kazi.ninapo waona wazee wa kigoma kukosa hata shilingi miamoja kununua chai asubuhi.Nina waona si wana Kigoma bali mamilioni ya Watanzania wakiishi kwenye hali hii.Alafu nalinganisha na Taarifa ninazo zipata kuhusu ufujaji na utoroshwaji wa Pesa zetu.Hebu sasa linganisheni na riporti ya kimataifa inayo sema hivi karibuni imeonyesha kuwa mwaka 2010 pekee jumla ya dola za kimarekani miliono1315(bilion1.3) yani shilingi Trioni 2113930000000(sh,Trion 2,1) Zilitoroshwa kutoka nchini Tanzania.Mwaka 2011kiasi cha dola za kimarekani milion 817 yaani shingi za Kitanzania Trion 1315370000000(Trioni 1.3) Zilitoroshwa nje ya nchi.Ripoti hiyo inaeleza kuwa jumla ya fedha za watanzania zilizo toroshwa nje ya nchi katika miaka kumi iliyo pita zilifikia dola za kimarekani 4526(bilion 4.5) sawa na shilingi za Kitanzania Triono7286860000000(Trion 7.3).Nime watajia hapa namba chungu nzima na matrioni na mabilioni hayaleti maana.Lakini hii ina maana kwamba kiasi cha fedha zilizo toroshwa katika miaka kumi Robo yake ttunge wez kujenga barabara yenye kiwango kizuri kabisa cha lami Kutoka Kigoma hadi Dar es Salaal! Pesa hizi zingeweza kuajiri na kuwalipa vizuri walimu,madaktari na wafanyakazi wengine ili kuhakikisha tuna pata huduma bora na kutengeneza ajira bora kwa vijana wetu.Pesa hiz zingeweza kununua dawa bora na muhimu na kuokoa maisha ya maelfu ya akina mama tulio wapoteza kila mwaka wakati wa Uzazi.Pesa hizi zingeweza kuwalipia watanzania si watoto tu angalau pea kumi ya viatu .Sasa nikitafakari haya siwezi kuuchapa usingizi mnono na kufumbia macho utoroshwaji wa fedha au matumizi mabaya ya fedha za umma kwasisi wabunge kujilipia posho, Hapana! Nfsi yangu hainiruhusu kukaa kimya kwa kuogopa kuitwa mbinafsi au msaliti.Lakini nina omba niwasihi katika kipindi kama hiki cha Changa moto za  kisiasa jambo la msingi kuliko yote ni kutulia maana hakuna linalo tokea bila sababu.Licha ya kwamba kuna wengi zaidiambao wako kimya lakini wana mawazo yao ndani na nje ya chama chetu ndani na nje ya Serikari yetu,ndani na nje ya nchi yetu.Ndiyo maana lazima kuibadili nchi yetu ili kuhakikisha kila raia anakuwa na fursa ya kutoa mawazo na fikra zake zina kuwa huru.Maisha ni Mabadiliko,Mabadiliko hayana ukomo,Mabadiliko haya zuiliki kwasababu bila mabadilko hakuana ukuaji,Bila mabadiliko hakuna maendeeleo.Mabadilko ni kiu kikubwa cha wa tanzania kwasababu mabadiliko huleta matumaini.Na kiu hii ni kubwa zaidi kwetu vijana wa kizazi hiki kipya.Siasa za kizazi kipya ni siasa za majawabu na kero za wana nchi.Siasa za mabadiliko ni siasa za kujenga na kuimarisha ni siasa za kuamianiana na kuheshimiana hata pale mnapo pingana kimawazo.Nina taka tujenge siasa mpya Tanzania,Siasa za mabadiliko;Siasa zinazo jenga matumaini ya kweli,Siasa zina zo wajali na kuwajengea uwezo wana nchi wa Tanzania.
MUNGU ibariki Tanzania.

Mjumbe
Mbeya

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top