Profesa Faustini Lekule
Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo (SUA),Kina hadharisha walaji wa nyama ya Nguruwe nchini kuwa wana kabiliwa na Hatari ya kupata Kifafa.Utafiti wa kisayansi Ulio fanywa SUA Umebaini kuwa baadhi ya nguruwe wana minyoo aina ya Tengu ambao nyama yao ikiliwa bila kuiva vizuri mlaji atapat minyoo hiyo ambayo huingia kichwani na Kusababisha KIFAFA.
Mhadhiri na mtafiti wa idara ya Sayansi ya Wanyama na Uzalishaji ya SUA,Profesa Faustine Lekule alisema sampuli za utafiti huo kutoka Mbeya zime baini nguruwe wengi wakiwemo wanao Safirishwa katika miji mikubwa wame athirika na minyoo Hiyo.
"Majibu ya sampuli ambazo wataalam wame zichukua kutoka kwa Nguruwe wa wafugaji kwenye baadhi ya vijiji wame bainika kukumbwa na Hatari hii,Lazima Jitihada zifanyike za kutafuta ufumbuzi wa Tatizo hili kati ya Watafiti,Wafugaji na Serikali";Alisema Profesa Lekule.
Kwa baadhi ya wafugaji wamekuwa wakijisaidia vichakani na kuwa Acha nguruwe kutafuta malisho katika vichaka na kula kinyesi chao hali hiyo huchangia ongezeko la maambukizi ya minyoo ya Tengu.
Mjumbe sr
Mbeya


Post a Comment