Unknown Unknown Author
Title: MJUMBE ATAKA JK APEWE TUZO YA KATIBA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Dodoma.   Mjumbe wa Bunge la Katiba, Yusuph Manyanga amependekeza Bunge hilo na Serikali kuandaa tuzo maalumu ya kumpatia aliyekuwa Mwe...



Dodoma. Mjumbe wa Bunge la Katiba, Yusuph Manyanga amependekeza Bunge hilo na Serikali kuandaa tuzo maalumu ya kumpatia aliyekuwa Mwenyekiti wa Muda wa Bunge hilo, Pandu Ameir Kificho.

Aliliambia gazeti hili kuwa pamoja na kuliendesha Bunge hilo bila kanuni, Kificho alilimudu na kufikia malengo yaliyokusudiwa kwa wakati ule.
Manyanga ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha Sauti ya Umma (SAU), alisema licha ya Kificho, pia tuzo apewe Rais Jakaya Kikwete kutokana na kuanzisha mchakato huo wa mabadiliko ya Katiba.
“Suala la kuandika Katiba katika mazingira ya amani siyo dogo, ni lazima tumpongeze Rais Kikwete kwa Tuzo ya Heshima, kwani ni busara zake tu ambazo zimewezesha jambo hili,” alisema Manyanga.
Kuhusu mchakato wa Katiba, alisema ni imani yake kuwa Katiba bora itapatikana, lakini akatoa wito wa wabunge na wawakilishi kutohodhi mijadala bungeni kwani hakuna aliye mzoefu katika Bunge la Katiba. 
Chanzo:Mwananchi
Mjumbe Jr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top