BAADHI ya abiria wanaotumia Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo (UBT),
wamesema afya zao ziko hatarini kwa kupatwa na magonjwa ya mlipuko
kutokana na kusambaa kinyesi kituoni hapo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Dar es
Salaam jana, abiria hao walisema licha ya Halmashauri ya Jiji kukusanya
ushuru kwa madai ya kukiweka kituo hicho katika hali ya mazingira ya
usafi, hali ni tofauti.
Walisema kusambaa kwa kinyesi na harufu mbaya ilitokana na kufumuka
chemba la majitaka kwa zaidi ya siku tano sasa, huku kukiwa hakuna
juhudi zinazofanyika kuondoa kero hiyo.
John Charles, ambaye ni abiria, alisema alishangaa kuwaona watendaji
wa jiji kufika katika eneo hilo huku wakishindwa kuchukua hatua za
haraka kwa ajili ya kulinda afya za abiria.
“Hali ni mbaya, tumewaona watu wa jiji walikuja na kuangalia kisha wakaondoka bila kufanya
chochote,” alisema.
Christina Donald, alishauri viongozi wanaohusika kuangalia kituo hicho na kuchukua hatua za haraka ili kunusuru afya za abiria.
Tanzania Daima
MJUMBE Sr
Post a Comment