MKUTANO NA WAANDISHI WA HABARI “PRESS CONFERENCE” TAREHE
19.06.2014.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
WATU WAWILI WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI USIKU WA KUAMKIA
LEO MAJIRA YA SAA 04:30 ALFAJIRIWALIONEKANA NA WALINZI WA USIKU WA ENEO LA SOKO
KUU LA TUNDUMA LILILOPO KATIKA KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA WAKIWA
NA SILAHA BUNDUKI NA KUWATILIA MASHAKA KUWA WANA NIA YA KUFANYA UHALIFU YAANI
UNYANG’ANYI WA KUTUMIA SILAHA.
WALINZI AMBAO WALIKUWEPO KATIKA ENEO HILO WALITOA TAARIFA
KWA ASKARI POLISI WALIOKUWA DORIA AMBAO WALIFIKA MARA MOJA KATIKA ENEO HILO.
KUTOKANA NA TAARIFA HIZO MSAKO MKALI ULIANZA KUWATAFUTA WATUHUMIWA HAO.
MNAMO MAJIRA YA SAA 05:00 ALFAJIRI YA LEO ASKARI POLISI
WALIKUTANA NA WATU WAWILI WALIOWATILIA SHAKA KUTOKANA NA JINSI WALIVYOVAA
KULINGANA NA MAELEKEZO YALIYOPEWA NA WALINZI.
MMOJA KATI YA MAJAMBAZI HAYO ALIKUWA AMEVAA JAKETI KUBWA JEUSI NA MWINGINE AKIWA AMEBEBA MFUKO MKUBWA, WAKATI WAKIJARIBU KUWASIMAMISHA WATU HAO WALIANZA KUKIMBIA NA MMOJA KATI YAO ALIYEKUWA AMEVAA JAKETI ALIPOFIKA UMBALI WAMITA 20 ALITOA SILAHA BUNDUKI NA KUANZA KUFYATUA RISASI OVYO AKIELEKEA UELEKEO WA ASKARI.
MMOJA KATI YA MAJAMBAZI HAYO ALIKUWA AMEVAA JAKETI KUBWA JEUSI NA MWINGINE AKIWA AMEBEBA MFUKO MKUBWA, WAKATI WAKIJARIBU KUWASIMAMISHA WATU HAO WALIANZA KUKIMBIA NA MMOJA KATI YAO ALIYEKUWA AMEVAA JAKETI ALIPOFIKA UMBALI WAMITA 20 ALITOA SILAHA BUNDUKI NA KUANZA KUFYATUA RISASI OVYO AKIELEKEA UELEKEO WA ASKARI.
BAADA YA KUONA HIVYO, ASKARI WALIJIBU NA KATIKA MAJIBIZANO
HAYO YA KURUSHIANA RISASI KATI YA
MAJAMBAZI NA ASKARI POLISI, JAMBAZI MWENYE SILAHA ALIPIGWA RISASI UBAVUNI
NA KUFARIKI DUNIA, HIVYO KUFANIKIWA
KUKAMATA BUNDUKI MOJA AINA YA AK- 47 YENYE NAMBA 592058 IKIWA NA RISASI 25
KWENYE MAGAZINE.
MTUHUMIWA MMOJA ALIFANIKIWA KUKIMBIA NA MARA BAADA YA
KUUPEKUA MWILI WA MAREHEMU KILIKUTWA KITAMBULISHO CHA MPIGA KURA CHENYE JINA
JOSEPH THADEI KAPINGA, MKAZI WA MAFIGA, MOROGORO ALIYEZALIWA MKOA WA RUVUMA –
SONGEA VIJIJINI TAREHE 07.09.1971.
KATIKA TUKIO HILO, HAKUNA MADHARA KWA WANANCHI/ASKARI
YALIYORIPOTIWA KUTOKEA, UPELELEZI UNAENDELEA IKIWA NI PAMOJA NA KUMTAFUTA
MTUHUMIWA ALIYEKIMBIA PAMOJA NA MTANDAO WAO WA UJAMBAZI.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MWANAMKE MMOJA ALIYETAMBULIKA KWA JINA LA SUZANE MHENDWA
(45) MKAZI WA UHAMILA WILAYANI MBARALI AMEUAWA KWA KUCHOMWA KISU KIFUANI NA MTU
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LAZARO KATENDE.TUKIO HILO LIMETOKEA USIKU WA KUAMKIA
LEO MAJIRA YA SAA 01:00 KATIKA KITONGOJI CHA CCM, KIJIJI CHA UHAMILA, KATA NA
TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA
TUKIO HILO NI MZOZO ULIOTOKEA KATI YA MAREHEMU NA MTUHUMIWA WAKIWA NYUMBANI
AMBAPO KIINI CHAKE KINACHUNGUZWA.
MAREHEMU NA MTUHUMIWA NI NDUGU WANAOISHI NYUMBA MOJA.
MTUHUMIWA ALIKIMBIA MARA BAADA YA TUKIO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISIAHMED Z. MSANGI
ANATOA WITO KWA JAMII/WANAFAMILIA KUTUMIA NJIA ZA BUSARA KATIKA KUTATUA
MIGOGORO KATIKA FAMILIA HASA KWA KUKAA MEZA MOJA YA MAZUNGUMZO ILI KUEPUKA MATATIZO.
AIDHA ANATOA WITO KWA MTU YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA
TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA
ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA TATU:
WATEMBEA KWA MIGUU WAWILI WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA 1.
THERESIA HINGI (65) NA 2. MARY KIZITO (26) WOTE WAKAZI WA IGURUSI WAMEFARIKI
DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA BASI LA KAMPUNI YA USAFIRISHAJI – NEW FORCE LENYE
NAMBA ZA USAJILI T. 952 CGU AINA YA SCANIA LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA YAHAYA
ABDALAH (39)MKAZI WA DSM.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 18.06.2014 MAJIRA YA SAA
18:00 JIONIKATIKA KIJIJI CHA IGURUSI, KATA YA IGURUSI, TARAFA YA ILONGO,
BARABARA KUU YA MBEYA/NJOMBE, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA
BASI HILO LILILOKUWA LIKITOKEA DSM KUELEKEA MBEYA MJINI LILIGONGA GARI T. 954
AMH AINA YA FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA TUPA ANYOSISYE (32) MKAZI WA
KIWIRA –TUKUYU, KISHA KUACHA NJIA NA KUWAGONGA WATEMBEA.
AIDHA KATIKA AJALI HIYO WATU WENGINE WANNE WALIJERUHIWA KATI
YAO ABIRIA MWANAUME MMOJA NA WANAWAKE WATATU WATEMBEA KWA MIGUU WOTE WAMELAZWA
KATIKA HOSPITALI YA MISHENI CHIMALA. PIA MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA
HOSPITALINI HAPO. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA BASI, AMBAYE
AMEKIMBIA MARA BAADA YA AJALI NA JUHUDI ZA KUMTAFUTA ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
MWANDAMIZI WA POLISIAHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI
WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA ALAMA NA SHERIA ZA USALAMA
BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA. AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA HUSIKA
ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
Imetolewa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment