Picha Na Maktaba ya MJUMBE BLOG(Ilipigwa Siku ya Uzinduzi wa Mradi wa Chuma wa Liganga,2013,Wapili kutoka kulia Ni Mkuu wa wilaya ya Ludewa,Ndg Solomon Juma Madaha)
ASKARI WA JESHI LA POLISI
ATOROKA LINDO AMUUA MWANANCHI KWA
RISASI WILAYANI LUDEWA KATIKA MKOA WA
NJOMBE.
Askari wa jeshi la Polisi kituo cha Ludewa mjini
ambaye alikuwa lindo la bank ya NMB mwenye
namba G.6352D/C aliyefahamika kwa jina moja la
Abduel anasadikika kumuua kwa kumpiga risasi na
bunduki aina ya SMG kijana mmoja aliyefahamika
kwa jina la January Mtitu (20) usiku wa kuamkia
tarehe 23/01/2015 nyumbani kwa kijana huyo.
Tukio hilo limetokea baada ya Askari huyo
kutoroka lindo na kwenda nyumbani kwa
marehemu maeneo ya Ludewa mjini mtaa wa
Mdonga usiku wa saa sita na kufanya uharifu huo
hali ambayo imewashtua wananchi wa mji wa
Ludewa ambao hawajawahi kuona matukio kama
hayo yakifanyika katika mji wao.
Hali hiyo imesababisha baadhi ya wananchi kutaka
kufanya maandamano ya amani kupinga kitendo
hicho cha kulaani jeshi la polisi kumuua
mwananchi asiye na hatia na pia wamesusia
kuchonga sanduku la kuuzika mwili wa marehemu
huyo wakitaka jeshi la polisi wilayani Ludewa
lihusike katika mazishi ya mwananchi huyo.
Akiongea kwa masikitiko mmoja wa mashuhuda
wa tukio hilo ambaye ni dada wa marehemu
January aliyejitambulisha kwa jina la Imani Mtitu
alisema marehemu alisikika akibishana na watu
katika simu yake ya mkononi kwa muda mrefu
majira ya saa sita usiku na baada ya mabishano
hayo watu hao walimweleza tunakuja huko kwako
naye akasikika akiwajibu njooni.
Imani alisema Baada ya dakika chache walisikika
watu akigonga mlango wa chumba cha kaka yake
na kuamua kuuvunja ndipo mabishano yakaendelea
huku marehemu akisikika kuwa anasema
anaadhibiwa kwa kosa asilolijua ndipo ikasikika
sauti ya risasi na marehemu akilalamika kwa
uchungu.
Baada ya kukamilisha tukio hilo alisikia vishindo
vya watu vikikimbia ndipo alipoamua kufungua
mlango wake bila mafanikio kwani ulikuwa
umefungwa kwa nje na wauaji hao akaamua
kutumia njia ya kutoka dirishani na kwenda katika
chumba cha kaka yake ambapo alimkuta akiwa
amelala chini na ametapakaa damu,alijaribu
kumuuluza ni akina nani waliofanyia tukio hilo
hakuweza kujibu kutokana na hali mbaya
aliyomkuta nayo ndipo alipoamua kuwaita majirani
na kuanza kuwafuatilia wauaji hao ambao
walionekana wakikimbia ikiwa moja amevaa sale
za jeshi la polisi na mwingine akiwa na mavazi ya
kiraia.
“nilisikia wakiongea tunakuua tupo tayari
kufukuzwa kazi mara iukasikika mlio wa bunduki
katika chumba cha marehemu kaka yangu
nilipojaribu kufungua mlango wangu ulikuwa
umefungwa kwa nje nakaamua kupitia dirishani na
kwenda haraka katika chumba cha kaka na
kumuona akiwa tayari hajitambui nikawaita
majirani kuwafuatilia wauaji tulifanyikwa kuwaona
watu wawili mmoja amevaa nguo za polisi na
mwingine nguo za kawaida wakikimbia”,alisema
Imani.
Alipo ulizwa mkuu wa wilaya ya Ludewa ambaye ni
mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama
Bw.Juma Solomon Madaha alithibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kuwataka wananchi kutuliza
jazba kwani bado uchunguzi kamili wa chanzo cha
tukio hilo unaendelea na baada ya kukamilika
wananchi watataarifiwa kuwa nini kinaendelea.
Endelea kufuatilia mtandao huu kujua nini
kinaendelea wilayani Ludewa.
Mwisho.
Tutembee MJUMBE BLOG M tandaoni Upate Picha,Matangazo,Matukio,Habari mpya kila mara.
Post a Comment