Noor Hassan
HII NDIYO CARTOON ILIOSABABISHA GAZETI LA
EAST AFRICAN KUPIGWA MARUFUKU TANZANIA
Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia idara ya Habari Maelezo imetangaza kupiga
marufuku usambazaji wa gazeti hilo nchini
Tanzania.
Kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi la na. 5298 la
januari 24,2015 limesema kwamba , Mkurugenzi
idara ya Habari Maelezo Assah Mwambene
amesema kuwa hatua hiyo imechukuliwa kufuatia
kutofurahishwa na jinsi gazeti hilo linavyoripoti
habari na uchambuzi wake hasa zinazohusu
Tanzania.
Mwambene alilituhumu gazeti hilo kuwa na
mtazamo hasi dhidi ya Tanzania. Alitoa mfano wa
maoni ya hivi karibuni ambayo yalikosoa msimamo
wa Serikali kuhusu waasi wa Rwanda, FDLR
walioko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
(DRC) kama mfano wa mtazamo wa gazeti dhidi
ya nchi
Mwambene pia alielezea katuni iliyotoka kwenye
toleo la wiki hii la The EastAfrican, kuwa ilionyesha
kutozingatia utamaduni na kwamba ilionyesha
kutomuheshimu Rais.
Katika Barua iliyotumwa kwa mwakilishi wa The
EastAfrican nchini, uamuzi huo umechukuliwa kwa
sababu gazeti hilo “limekuwa likisambazwa nchini
bila ya kuwa na usajili, kinyume na kifungu cha 6
cha Sheria ya Magazeti, Namba 3 ya mwaka
1976”.
Uongozi wa Nation Media Group, ambao unamiliki
gazeti la The EastAfrican, umeelezea hatua hiyo
kuwa ni ya kushangaza na isiyokubalika. Barua
hiyo ya Januari 21, 2015 inaagiza kusimamishwa
mara moja kwa uchapishaji na usambazaji wa
gazeti hilo nchini Tanzania ‘’hadi litakaposajiliwa
rasmi na Msajili wa Magazeti, Idara ya Habari’’.
Kabla ya kutolewa kwa barua hiyo, mwakilishi wa
gazeti hilo nchini, Christopher Kidanka aliitwa
Jumatano na kuhojiwa na mkurugenzi wa Idara ya
Habari.
Akizungumzia uamuzi huo wa Serikali, mwenyekiti
wa Bodi ya NMG Group, Wilfred Kiboro alisema
sababu zilizotolewa na Serikali zinashangaza kwa
sababu gazeti hilo limekuwa likisambazwa tangu
miaka 20 iliyopita.
Alisema kwamba sababu halisi “ziko sehemu
nyingine “ na zinaweza tu kuhusishwa na
msimamo wa gazeti hilo, na mengine ya kampuni
NMG, limechukua katika kuripoti rushwa, wizi wa
mali za umma na utoaji duni wa huduma kwa watu
wa Afrika Mashariki.
Tutembelee MJUMBE BLOG mtandaoni kwa picha,Habari mpya,Matangazo na Matukio kutoka kila kona.
Post a Comment