Unknown Unknown Author
Title: KAULI YA MWIGULU NCHEMBA MARA TU BAADA YA KUPIGWA STOP KUFANYA ZIARA ZAKE MIKOANI!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania Bara), Mwigulu Nchemba amekubali kuitikia wito wa kusitisha ziara zake za kichama katika mikoa na wi...

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM (Tanzania
Bara), Mwigulu Nchemba amekubali
kuitikia wito wa kusitisha ziara
zake za kichama katika mikoa na
wilaya mbalimbali nchini, kama
alivyoagizwa na Katibu Mkuu wa chama
hicho, Abdulrahman Kinana.
Katika barua yake ya Januari 18,
mwaka huu, Kinana alimwagiza Mwigulu
ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha
na Mbunge wa Jimbo la Iramba
Magharibi mkoani Singida, kusitisha
mara moja ziara zote na kwamba
endapo atataka kufanya hivyo,
atalazimika kutoa taarifa na kupata
kibali.
Akizungumza jana na gazeti hili,
Mwigulu alikiri kupokea barua hiyo,
na kusema hana tatizo na kusitisha
ziara zake za kichama, kwani ni
maagizo halali ya mamlaka ya juu
yake kichama.
“Haya ni maelekezo, na siku zote kwa
kuwa nafanya kazi kwa mujibu wa
Katiba, sioni tatizo kupokea
maelekezo rasmi ya kiofisi…
aliyeniagiza ni kiongozi wangu katika
chama, nitafanya hivyo,” alisema
kiongozi huyo kijana, lakini
machachari katika ulingo wa siasa.
Katika siku za hivi karibuni,
amekuwa akipasua anga kwa kutumia
helikopta katika ziara zake
alizofanya mikoa ya Tanga na
Morogoro.
Mwigulu alisema amekuwa akipokea
mialiko mingi ya kichama, hivyo
anajikuta akitumia muda wake wa
ziada wa siku za mwishoni mwa wiki
kufanya ziara, lengo likiwa
kutenganisha muda wa utendaji wake
katika chama na serikalini.
“Ndiyo maana nilikuwa nafanya ziara
za kichama siku za mwisho wa wiki
pekee…na baada ya Morogoro pia
nimealikwa Kigoma, Mafia (Pwani),
Kagera, mikoa ya Kusini na Njombe.
Kwa ujumla mialiko ni mingi, lakini
nitaifanya kwa kufuata maelekezo.
“Sitavunja sheria za chama wala za
nchi hata siku moja, nitawatumikia
wananchi kwa mujibu wa taratibu
zilizowekwa,” alisisitiza Mwigulu.
Barua hiyo ambayo Kinana alimwandikia
Mwigulu tarehe 18 Januari mwaka huu,
mwaka huu ilisomeka hivi: “Umekuwa
ukifanya ziara nyingi katika mikoa
na wilaya bila ushirikishwaji kamili
wa Makao Makuu, Mikoa na hasa Kamati
za Siasa. Wewe pia umeonesha kwa
kauli na mienendo yako kujiandaa
kugombea nafasi ya Urais kupitia
CCM. Ziara hizi zina mwelekeo wa
kampeni, jambo ambalo ni kinyume na
maadili ya Chama. Nakuagiza
kuzisitisha ziara zote. Iwapo
utataka kufanya ziara yoyote ya
Kichama itabidi kwanza uniarifu na
upate kibali changu. Nakuagiza
utekeleze agizo hili mara moja”.
Hata hivyo, mara zote alizoulizwa
kuhusu kuwania Urais mwaka huu,
Mwigulu amekuwa haweki wazi dhamira
hiyo kama inavyoelekezwa.
Lakini, amekuwa akisisitiza amekuwa
akiombwa kufanya hivyo na makundi ya
watu mbalimbali, wakiwemo wanasiasa,
wasomi, wakulima na wafanyakazi,
vijana, wazee, wanawake na wanaume.
HABARI LEO

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top