Mahakama ya wilaya ya ludewa mkoa wa
njombe imewasomea mashitaka
watuhumiwa watatu pamoja na aliyekuwa
askari wa jeshi la polisi wa kituo cha
ludewa mjini mwenye namba G, 6352
Abduel Amza Nyuki mwenye umri wa
miaka 3o, Juma mhagama 21 pamoja na
Rashidi amadi wote wakazi wa mtaa wa
ibani ludewa mjini kwa kesi ya mauwaji
kinyume na kifungu cha sheria cha 196
kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Na Maiko Luoga Ludewa ,Mahakama ya
wilaya ya ludewa mkoa wa njombe
imewasomea mashitaka watuhumiwa
watatu pamoja na aliyekuwa askari wa
jeshi la polisi wa kituo cha ludewa mjini
mwenye namba G, 6352 Abduel Amza
Nyuki mwenye umri wa miaka 3o, Juma
mhagama 21 pamoja na Rashidi amadi
wote wakazi wa mtaa wa ibani ludewa
mjini kwa kesi ya mauwaji kinyume na
kifungu cha sheria cha 196 kilichofanyiwa
marekebisho mwaka 2002.
Kesi hiyo imesomwa January 26 na Wakili
Edward Mohamed mtahiruka mbele ya
hakimu wa wilaya Fredrick lukuna na
kusema kuwa tukio hilo lilifanyika usiku wa
kuamkia january 23.2015 majira ya saa
sita kamili usiku katika mtaa wa mdonga
wilayani Ludewa ambapo watuhumiwa hao
wanashitakiwa kwa kosa la Mauaji ya
January mtitu aliyekuwa na umri wa miaka
20 .
Wakili huyo alisema kuwa Aliyekuwa askari
wa jeshi lapolisi ludewa mjini Bw, Abduel
Nyuki ndiye aliye kuwa muhusika wa
kufanya ,auaji hayo kwa kutumia risasi
mnamo usiku wa kuamkia january 23 saa
sita usiku kwakuambatana na vijana hao
wawili ambao walimpeleka mtuhumiwa
huyo nyumbani kwa marehemu na kwenda
kufanya mauaji hayo.
Hata hivyo watuhumiwa hao
hawakuruhusiwa kujibu chochote na kuwa
keso hiyo imeahirishwa hadi tarehe
2.2.2015 Hivyo watuhumiwa
wamerudishwa mahabusu kwakuwa kesi
yao haina mdhamana.
Picha Na Mwalimu Mahenge JJ
MJUMBE BLOG tunapatikana Mtandaoni kwa picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu na matukio yanayo gonga vichwa vya habari kila kona!
Post a Comment