Mwanamke mmoja mkoa Tabora wilaya ya
Tabora mjin kata ya chemchem amewaua
watoto wake 2 na kuwazika ndani ya NYUMBA
yake.
==========================
Mume kamkimbia maisha akayaona magumu,
akawalisha sumu na walivyokufa akaanza
kuchimba hilo shimo, kuna jirani alimsikia
akichimba lakini akampuuza. Siku ya pili
akatangaza kupotelewa na watoto ila yule jirani
akaliwekea mashaka na akatoa taarifa polisi
kwamba kuna siku alimsikia muhusika kama
alikuwa anachimba usiku na siku hiyo aliwaona
watoto wake wote wakiingia ndani kwao kwani
mara ya mwisho walikuwa kwake wakicheza
mpaka giza lilipoingia ndio akawaamuru warudi
nyumbani.
Dotto Mnzava :
Katika hali isiyotegemewa watoto wawili
wameuawa na mama yao , Zuhura Steven,
anayedhaniwa kuwa anaupungufu wa akili na
kufukiwa katika mashimo mawili tofauti, katika
nyumba walimokuwa wakiishi, katika Mtaa wa
Salimini Kata ya Chemchemu Manispaa ya
Tabora.
Wakizungumzia tukio hilo linalodhaniwa
kutokea kuanzia asubuhi ya Januari 25,2015,
hadi majirani walipogundua tukio hilo usiku
jana, Mwenyekiti wa Mtaa wa Barehani pamoja
na wananchi walioshuhudia tukio hilo
wanasema kuwa mchana watoto hao
hawakuonekana kama mazoea yao ambapo
wamekuwa wakionekana kila siku nyakati za
mchana wakicheza.
Jeshi la Polisi mkoani Tabora limethibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kuwataja marehemu
kwa majina ya Mwamvua Mrisho (4) na Soud,
(miezi 4) na upelelezi unaendelea pindi
utakapokamilika mtuhumiwa atafikishwa
Mahakamani.
Chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana na
mtuhumiwa yuko mikononi mwa polisi hadi
sasa.
Tutembelee MJUMBE BLOG Mtandaoni kwa picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu na matukio yaliyo gonga vichwa vya habari.
Post a Comment