Watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi,
wamewavamia na kuwajeruhi askari mwenye no
G369 PC Mansour na Hv507 PC Mwalimu,
wakiwa doria ya pikipiki ambao
walinyang'anywa silaha mbili aina ya SMG no
14301230 na 14303545 na watu wasio julikana
mkoani Tanga.
Taarifa ya Jeshi hilo kwa vyombo vya habari
imesema tukio hilo limetokea Januari 26, 2015
majira ya saa 23:30hrs eneo la barabara 04 jijini
humo.
Aidha, imesema mmoja wa majeuhi askari
mmoja no H 507 PC Mansour amejeruhiwa
vibaya maeneo mbalimbali ya mwili na
amelazwa katika Hospitali ya Mkoa Bombo.
Katika uchunguzi wa awali Polisi wamefanikiwa
kumtia hatia hatiani mtuhumiwa mmoja, Ayubu
Haule, (27), fundi Radio Mkazi waCorner Z
Amboni Kiomoni ambaye alikamatwa eneo la
tukio akijaribu kutoroka na pikipiki na mara
baada ya kupekuliwa ndipo alipokutwa na
mchoro wa ramani unaoonyesha matokeo ya
Barabara na kufunguliwa kesi yenye no TAN/
IR/322/2015.
Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na Jeshi hilo
huku timu ya Intel na makachero wa Polisi
ikiendelea kufanya doria pamoja na Section 2 za
FFU.
Post a Comment