Safari za ‘’comandante’’ Che Guevara nchini
Tanzania zinaweza kugawanywa kwenye awamu
mbili.
Kwenye safari yake ya kwanza, aliingia
Tanzania tarehe 11, Februari 1965. Akiwa Tanzania
aliongea na wawakilishi na viongozi mbalimbali wa
vikundi vya kupigania uhuru kama vile vya Kongo
na Msumbiji (Tazama pichani akiwa na Eduardo
Mondlane wa FRELIMO).
Kupitia mazungumzo
yake na vikundi hivi, Che alishawishika kushiriki
harakati ya waasi wa Kongo chini ya Kabila
(baba).
Che aliondoka Dar akiwa na furaha ya kuwapata
wapiganaji waliokuwa tayari kupambana kwa ajili
ya ukombozi. Kwa maneno ya mwandishi Piero
Giejesses ‘’Che left Dar filled with the joy of having
found people ready to fight to the finish and the
next task was to select a group of Black Cubans-
all volunteers to join the struggles in Zaire’’(Rejea
kitabu chake cha Conflicting Missions: Havana,
Washngton and Africa)
Safari ya pili ya Guevara nchini Tanzania aliifanya
mwezi Aprili 1965. Guevara, akiwa na Askari
wengine wa Ki-Cuba ( Wengi Wa-cuba weusi)
walikuwa wamejipanga tayari kwenda kwenye
uwanja wa mapambano nchini Kongo. Che Guevara
alikuwa amejibadilisha kiasi kwamba hata
mwenyeji wake (Balozi wa Cuba nchini)
hakumtambua. Kwa maneno yake mwenyewe
(Kwenye kitabu chake cha The African Dream)
Guevara anasema ‘’One fine day, I appeared in Dar
es salaam. Nobody knew me; not even the very
ambassador (Pablo Ribalta) an old comrade in
arms..’’ Badala ya kujiita majina yao, Guevara na
makomredi wenzake walijipa majina kijasusi kwa
mtindo wa namba za Kiswahili. Guevara alijiita
tatu!
Guevara alirudi tena Dar baada ya operesheni yake
ya Kongo kufeli. Kati ya mwezi Novemba 1965 hadi
Februari 1966, Guevara aliishi Dar kwenye ubalozi
wa Cuba mtaa wa Upanga. Katika kipindi hiki,
Guevara aliichambua na kuitathmini harakati yake
nchini Kongo. Kumbukumbu alizoziandika katika
kipindi hiki zimechapishwa kwenye kitabu chake
maarufu kuhusu harakati yake ya Kongo kiitwacho
‘’African Dream: The Diaries of the Revolutionary
War in Congo’’.
Kwa maoni ya Guevara (kama alivyonukuliwa na
George Castaneda kwenye kitabu cha
‘’Companero’’) kulikuwa na tatizo kubwa la
kioganaizesheni na stratejia kwenye jeshi la Kabila.
Nikiazima maneno yake mwenyewe (uk 308)..''the
main defect in the Congolese is that they dont
know how to shoot..Discipline here is very
poor..the main feature of the People's Liberation
Army( kabila's Army) is that it was a parasite
army which didnt work, didnt train, didnt fight and
demanded supplies and labor from the population,
sometimes by force''.
Halafu pia hakukuwa na umakini kwa upande wa
viongozi wa waasi. Kina Kabila waliendekeza sana
starehe. Guevara anasema ‘’The majority of African
rebels live comfortably in hotels and have turned
rebellion into a profession, at times lucrative and
almost always comfortable..’’ Castaneda
anaongezea kwenye kitabu chake (uk
307
''..Neither Kabila nor his deputies were in any
position to lead: not only were absent most of the
time, they lacked capacity. And there was nothing
Che could do: he was not the leader''
Lakini Che aliamini Kabila alikosa umakini
kutokana na umri wake mdogo (Chini ya miaka
30). Aliamini miaka ya baadaye angekomaa
kiharakati na kumng’oa Mobutu. Kama wote
tujuavyo, ubashiri huu wa Che ulitimia. Kwa
maneno yake mwenyewe Che anasema ‘’
''It is
essential to have revolutionary seriousness, an
ideology that can guide action, a spirit of sacrifice
that accompanies one's actions. Up to now, kabila
has not shown that he posseses any of these
qualities. HE IS YOUNG and it is possible that he
will change''
kuhusu safari ya
Guevara akiwa Zanzibar tulichokitoa kwenye kitabu
cha Don Peterson Kiitwacho ‘’Zanzibar Revolution:
An American Cold War Tale’’. Kwenye kifungu
tulichokinukuu Peterson, mwanadiplomasia wa
kimarekani aliyekuwepo Zanzibar wakati wa
mapinduzi ya Zanzibar anasimulia jinsi
alivyokutana na Guevara Zanzibar kwenye sherehe
ya mapinduzi mwaka 1965. Kwa Kiingereza kifungu
chenyewe kinasomeka ifuatavyo:
‘’ I sat behind karume and his notable guest, the
famous cuban revolutionary, Che Guevara at the
football stadium during a bull fight part of
Zanzibar's and Pemba's portuguese heritage
Guevara was at the state ball that night. At one
point he said helo to (my wife) Julie and he was
delighted when she responded in spanish. He
asked her where she was from and when she told
him , he said ‘’that’s nice a girl from Mexico. What
are you doing here?
‘’My husband is the American Consul’’ she
answered. Guevara’s mouth dropped open; he
stared for a moment the without further word
turned around and walked away.’’ (uk 253).
Legacy:
'Ernesto Che Guevara ameacha urithi mkubwa
sana Afrika. Picha yake imekuwa ikitumika sana
kama ishara ya kupinga unyanyasaji na pia
kuhamasisha mapinduzi. Wakati wa mapinduzi ya
Yasmini yaliyoanzia Tunisia na kuendelea Misri, na
Libya kwa sehemu kubwa vijana walioshiriki
mapinduzi yale walikuwa wamevaa mikufu na
fulana zenye picha ya Che Guevara. Che Guevara
amekuwa akitumika kama sauti ya wanyonge. Hili
linajidhihirisha alipoamua kujiunga na waliotaka
kuiondoa serikali ya Zaire (sasa Congo-DRC).
Hakuonesha kupendezwa na ubaguzi wa rangi na
unyanyasaji wa watu weusi waliokuwa wakidai
haki zao za halali hasa kupitia hotuba yake
aliyoitoa katika mkutano wa Umoja wa Mataifa
mwaka 1964.'
Pichani: Che Guevara akiwa Zanzibar..Unamt
ambua mwenye suti nyeupe aliye pembani kwa
Guevara?
Credit:Kitabu Nilicho Soma.
MJUMBE BLOG
Tuna Shukuru kwa Kututembelea .
Post a Comment