Unknown Unknown Author
Title: VYAMA VYA SIASA VYAONYWA DAFTARI LA KUDUMU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
SERIKALI ya wilaya Masasi mkoani Mtwara imevitaka vyama vya siasa kupitia mawakala wao wasiingilie kazi za utendaji wakati wa kuandikish...

SERIKALI ya wilaya Masasi mkoani
Mtwara imevitaka vyama vya siasa kupitia
mawakala wao wasiingilie kazi za utendaji
wakati wa kuandikisha na kuboresha
daftari la kudumu la wapiga kura kwa
wananchi, mwaka huu.
Agizo hilo lilitolewa mwishoni mwa wiki na
Farida Mgomi wakati wa kufungua semina
ya wasaidizi waandishi, maofisa uchaguzi
kutoka kwenye kata mbalimbali wilayani
Masasi, inayoendeshwa na ofisi ya tume
ya uchaguzi ya Taifa.
Alisema uingiliaji huo wa mawakala
unaweza kuleta matatizo ya uvunjaji wa
amani, wakati wa uandikishaji na
uboreshaji wa daftari hilo.
Alisema Serikali ya wilaya nayo
itahakikisha uchaguzi unafanyika bila ya
kuwapo malalamiko yoyote yale kwa
upande wowote ule wa vyama vya siasa
au kwa mwananchi.
Aidha aliwataka waandishi wasaidizi wa
daftari la kudumu la wapiga kura kwa
kutumia teknolojia ya kompyuta (BVR)
kuwa makini na mafunzo hayo, ili kuweza
kutoa huduma stahiki kwa wateja wao
kipindi cha uchaguzi, mwaka huu.



MJUMBE BLOG
Tunakupongeza kwa kutumia huduma zetu.
HONGERA.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top